UONGOZI Wa Majimaji kupitia kwa Mwenyekiti Humphrey Millanzi wamesema mkataba wao na Symbion ambayo ni kampuni ya kufua umeme umemalizika rasmi na hawatakuwa Nao tena katika msimu ujao.
Mh.Diwani wa kata ya Misufini Ismail Aziz Fakir akidadisi jambo kwenye mkutano huo |
Akizungumza mbele ya wadau,wanachama,wapenzi na mashabiki wa Majimaji Mjini Songea katika uwanja wa majimaji jioni ya leo Millanzi amesema kuwa symbion kutokana na matatizo waliyoyapata ya kuvunjika kwa mkataba baina yao na Serikali wameamua pia kuvunja mkataba na clabu yao.
Mwenyekiti wa klabu ya Majimaji Humphurey Milanzi akifuatilia kwa makini na kuzisikiliza hoja za wajumbe waliohudhuria mkutano. |
"Majimaji hatutakuwa na Symbion tena msimu ujao sababu na wao wamepata matatizo Serikalini hivyo na wao mkataba wao unakaribia kuvunjwa hivyo basi tumeona tulilete hili hapa kwenu wadau ili tuangalie ni jinsi gani tunaweza tukashauriana katika hili maana hatuna mdhamini mkuu ambaye tulikuwa tunamtarajia na aliyekuwa nasi katika msimu uliopita na hata Majimaji ikiweza kusimamama kama ilivyo mpaka hivi sasa".Alisema Mwenyekiti Millanzi.
Mh. Diwani wa kata ya Limamu Isdory Brown Nyati "Mdolino" akiwa na Celvin Challe wakifuatilia kwa umakini mijadala mbalimbali iliyokua ikiendekea kwenye mkutano huo. |
Aidha Mwenyekiti huyo ameongeza kwa kusema kuwa wametuma maombi sehemu mbali mbali ikiwemo ndani na nje ya mkoa wa Ruvuma kwa ajili ya kuangalia ni jinsi gani wanaweza kupata Sapoti kwa ajili ya timu hiyo iweze kushiriki vyema mashindano ya ligi kuu msimu ujao.
Said Moyo mmoja kati ya wanachama machachari wa klabu ya majimaji akifuatilia kwa makini mjadala. |
Kwa upande mwingine Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Ruvuma (FARU)Golden Sanga alisema kuwa inabidi uongozi wa Majimaji uketi na bodi yake uzungumze kwa undani zaidi juu ya madeni ambayo iko nayo lakini pia lazime iangalie kwa haraka zaidi kuhusiana na usajili ili kuinusuru timu isishuke daraja kwani timu hii ilipo sasa hivi si ya kumsusia mtu ni ya kwetu sote.
Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Ruvuma Golden Sanga "Sanga One" nae alikua ni mmoja wa wajumbe waliohudhuria kwenye kikao hicho. |
Hata hivyo Mkutano huo ulivunjwa na mwenyekiti Millanzi baada ya kutokuwa na masikilizano kati ya uongozi uliopo katika mkutano huo na wadau waliojitokeza katika mkutano huo.
Post a Comment