0
Mshambuliaji hatari wa Yanga, Amissi Tambwe huenda akaukosa mchezo wa Jumamosi dhidi ya Madeama ya Ghana kutokana na kulazwa Hospitali akisumbuliwa na Malaria.

Meneja wa Yanga Hafidhi Salehe, amesema, mchezaji huyo amelazwa jana mchana na amepatiwa huduma ya drip na ameanza kupata nafuu.

“Bado hatujajua hadi Jumamosi hali yake itakuwaje lakini kwasasa anaendelea vizuri kiasi ingawa bado yupo Hospitali kwa ajili ya uangalizi wa karibu kutoka kwa Madaktari wetu na Hospital ya Aghan,”amesema Salehe.

Yanga itakuwa nyumbani Jumamosi kuwakabili Madeama, ya Ghana ukiwa ni mchezo wa tatu wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika CAF.

Post a Comment

 
Top