Nahodha wa timu ya Manchester United Wayne Rooney amemsifia kocha
wake mpya Jose Mourinho na kudai kuwa atairudisha Man Utd katika makali
yake.
Rooney mwenye miaka 30, anasema anamfahamu Mourinho kama moja ya
mameneja bora zaidi ulimwenguni kwa sasa na anatarajia atairudisha timu
yake ya Manchester United kama ilivyokuwa hapo awali chini ya Fergerson.
Kocha Jose Mourinho tayari alishaweka bayana dhamira yake ya
kumchezesha mshambuliaji huyo katika nafasi ya ushambuliaji wa mbele
tofauti na meneja aliyepita bwana Louis Van Gaal aliyekuwa akimtumia
Rooney kama kiungo mshambuliaji.
Rooney amekuwa akitumika kama kiungo mshambuliaji katika kikosi cha
United na cha timu ya Taifa ya Uingereza chini ya Hodgson ambaye
amejiuzulu nafasi hiyo baada ya kutolewa mapema katika michuano ya Euro
huko Ufaransa.
“Najisikia ni mwenye furaha kufanya kazi na Jose msimu huu, na mmoja
kati ya mameneja bora Zaidi ulimwenguni” alisikika Rooney akiongea na Inside United.
“Nimecheza dhidi ya timu nyingi zilizofundishwa na Mourinho,
wala sikumbuki mechi rahisi kati ya hizo, timu zote zilikuwa ngumu
kuzifunga, na zilikuwa nzuri kimbinu pamoja na kiuchezaji” aliongeza
Rooney.
Post a Comment