MWENYEKITI wa Chama cha wasakata kabumbu waliostaafu Mkoani Ruvuma (Sputanza) John Kabisama amesema kuwa wapo tayari kabisa kwa uchaguzi wao ambao unatarajia kufanyika tarehe 30 ya mwezi huu.
Akizungumza na Kipindi cha michezo leo cha Jogoo Fm ya Mjini Songea Mwanandinga huyo wa zamani wa Majimaji na Ushirika ya Moshi amesema kuwa kila kitu kipo sawa na fomu zinapatikana kwa kamati huru ya uchaguzi chini ya Wakili Abel Ngilangwa ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati huru ya Uchaguzi.
"Kwa taarifa tu ni kwamba tarehe 30 ndiyo siku ambayo Chaguzi zote za vyama Shirikishi mkoani Ruvuma zinatakiwa ziwe zimefanyika na hii ni kutokana na walaka tulioupata kutoka Tff na Faru(Chama cha Soka mkoa wa Ruvuma).
Kwa kuzingatia hilo sisi kama Sputanza nikiwa mwenyikiti na katibu wangu tulikaa na kutengeneza taratibu zote za uchaguzi huo utakavyofanyika na hivyo basi taratibu zote zipo sawa ikiwemo kamati huru ya uchaguzi"Alisema Kabisama ambaye ni mwenyekiti wa Sputanza Mkoani Ruvuma.
Aidha amemtaja Abel Ngilangwa (Wakili)kuwa ndiye mwenyekiti wa kamati huru ya uchaguzi akisaidiwa na Katibu Ajaba Chitete,na kwa yeyote aliye tayari basi awatafute kati ya hao ili aweze kupata Fomu yake kisha ajaze na gharama ya fomu ni shillingi elfu tano tu(5000/=).
Post a Comment