Afisa habari wa klabu ya yanga aliyefungiwa kwa kipindi cha mwaka mmoja na TFF kujihusisha na maswala ya mpira wa miguu Jerry Muro amesema haitambui adhabu hiyo na anajiandaa kushuka na majibu ambayo mwenyewe ameyaita moto wa kuotea mbali anayotarajia kuwajibu mabosi hao wa TFF.
Muro amesema haitambui adhabu hiyo na hivyo hatokata rufaa na badala yake anatarajia kukutana na waajiri wake mabosi wa klabu ya Yanga ili kupata muongozo kabla ya kutoka na kauli juu ya maamuzi hayo ya kamati ya maadili.
"Mwajili wangu mimi ni Yanga hivyo yeye akitaka nikae pembeni na nisijihusishe na masuala ya mpira nitakaa pembeni na sita jihusisha sio viongozi wa TFF wao hawana ubavu wakunizuia mimi kufanya shughuli zangu za ndani ya Yanga"
"Mwajiri wangu aliyekua akinituma nipambane kwaajili ya Yanga akiniamuru nikae pembeni nitakaa pembeni na ndio maana nimekua nikisisitiza kuwa mimi namsikiliza mwajiri wangu yeye akiniambia nikae pembeni hakuna shaka nitakaa pembeni"
Post a Comment