MVULA ndondo Cup inatarajia kuendelea siku ya Jumapili ya tarehe 17/07/2016 katika uwanja wa Sokoine uliopo kata ya Bomba mbili katika hatua ya kumi na mbili bora baada ya kumalizika kwa hatua ya Mtoano.
Akizungumza mara baada ya zoezi la uokotaji wa kuponi lililofanyika katika ofisi ya Chama cha soka Manispaa ya Songea (Sufa) Godfrey Ambrosy Mvula amesema kuwa kila kitu kipo sawa na amewataka wapenzi wa Soka kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Sokoine kuendelea kupata burudani ambayo ilisimama kwa siku kadhaa.
"Kwanza napenda kuwashukuru vilabu vyote kwa kushirikiana kumaliza zoezi hili la kuokota kuponi salama lakini niwaombe tu wadau na wapenzi wa soka kuendelea kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Sokoine kuanzia jumapili ya tarehe 17 July na kuendelea"Alisema Mvullah ambaye ni Mdhamini wa mashindano hayo.
Aidha Mvullah amevitaka Vilabu hivyo kujiandaa vya kutosha katika hatua ya kumi na mbili bora kwani hatua hii ni ngumu zaidi na kila timu inatakiwa kujipanga vilivyo ili kufanya vizuri zaidi.
Vilabu vilivyofuzu hatua ya kumi na mbili bora ni Pamoja na Bomba mbili fc,Stand fc, Ruvuma Chini fc,Mchikichini fc,Tembele fc,Mgundini fc,Lizabon City,Lizabon Junior,Mlimani fc,Walifa fc na Elimu Manispaa fc.
Na hii hapa ni ratiba ya 12 bora baada ya droo kuchezeshwa Alhamisi ya tarehe 14 July.
Tarehe 17/07/2016
Bomba mbili Vs Manispaa.
Tarehe 18/07/2016.
Stand fc Vs Ruvuma Chini.
Tarehe 19/07/2016
Mchikichini Vs Tembele.
Tarehe 20/07/2016.
City Center Vs Mgundini.
Tarehe 21/07/2016.
Lizabon City Vs Mlimani.
Tarehe 22/07/2016.
Walifa Vs Lizabon Junior.
Bomba mbili Vs Manispaa.
Tarehe 18/07/2016.
Stand fc Vs Ruvuma Chini.
Tarehe 19/07/2016
Mchikichini Vs Tembele.
Tarehe 20/07/2016.
City Center Vs Mgundini.
Tarehe 21/07/2016.
Lizabon City Vs Mlimani.
Tarehe 22/07/2016.
Walifa Vs Lizabon Junior.
Post a Comment