Washiriki wa majimaji selebuka katika upande wa ngoma za asili wakifanya yao kwa udadisi na umahiri mkubwa kabisa!
Ikiwa ni siku ya pili tangu kufunguliwa kwa tamasha la majimaji selebuka,mashindano mbalimbali yamezidi kushika kasi,vikundi mbalimbali vimejitokeza katika mashindano hayo vikiwemo vikundi vya ngoma ya asili mkoani ruvuma,lakini pia kumekuwa na muitikio mkubwa kwa upande wa wananchi na wa mkoani hapa,mashindano mbalimbali yanafanyika katika viwanja hivi ikiwa pamoja na mbio ndefu za miguu,lakini pia mashindano ya baiskeli pamoja na mashindano ya ngoma za asili ambapo hii leo vikundi mbalimbali vimeingia katika fainali na hatimaye mshindi kutangazwa hapo kesho.
hapo jana, Tamasha hilo lilikata utepe jana Mei 28 na litafika tamati Juni 4, mwaka huu na linaganyika kwenye Uwanja wa Makumbusho ya Mashujaa wa Vita vya Majimaji mjini Songea, Ruvuma
Judith alitumia muda wa dakika 27:28, akifuatiwa na Fatuma Ching’ang’a aliyetumia dakika 28:46 huku Theresia Tembo akimaliza wa tatu akihitimisha kwa muda wa dakika 30:26.
Akizungumzia ushindi wake, Judith alisema siri ya ushindi kuwa ni mazoezi kila siku, kupumzika muda mrefu na mlo mzuri.
“Tofauti na Jumapili kila siku nafanya mazoezi nazunguka uwanja wa mara tano, sinywi pombe, nalala muda wa kutosha (masaa 8) na kula vizuri (diet) ndiyo maana nimeweza achilia mbali umri wangu kunitupa mkono (miaka 38),” alisema Judith.
Kwa upande wa wanaume, kinara alikuwa Hamad Rashid aliyetumia dakika 16:59, nafasi ya pili Ferdinand Haule aliyetumia dakika 18:22 wakati nafasi ya tatu ilichukuliwa na Nathan Mpangala aliyetumia dakika 29:19 ambaye mbali na ushiriki huo, pia ni balozi wa tamasha.
Katika mbio za Km 21, John Mahagula aliibuka kinara kwa kutumia muda wa saa 1:32: 14, Jackson Faustine nafasi ya pili saa 1:41:17 na nafasi ya tatu ilichukuliwa na Abdallah Oscar aliyetumia muda wa saa 1: 50:48.
mashindano zaidi yanaendelea katika viwanja hivyo hivyo ni rai kwa wakazi wa Ruvuma kujitokeza kwa wingi zaidi hapo kesho!!
Post a Comment