Klabu ya SimbaSC ilikuwa kwenye machakato wa kumpa kazi ya Ukurugenzi wa Ufundi kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania Hemed Suleiman Ally ‘Morocco’, dili hilo lemeenda mrama baada ya wekundu wa Msimbazi kushindwa kuafikiana na Morocco juu ya kiwango cha mshahara.
Mwanzoni Morocco alikubaliana na uongozi wa Simba tangu wakiwa
visiwani Zanzibar wakati Simba ilipokuwa ikishiriki mashindano ya
Mapinduzi hadi Morocco akafunga safari ya kuja Dar es Salaam kumalizia
vipengele vichache ili ajiunge na timu.
Lakini ghafla uongozi wa Simba ukabadili maamuzi ya kiwango cha mshahara ambao walikuwa wamekubaliana mwazo.
Awali Morocco alikubaliana na uongozi wa Simba kwamba, watakuwa
wakimlipa Shilingi za Kitanzania 5,000,000 kwa mwezi, lakini baadaye
wakabadilisha maamuzi na kumwambia Morocco watakuwa wakimlipa 4,000,000
kwa mwezi.
Kuona hivyo Morocco akaamua kupiga chini dili hilo kutokana na
uongozi wa Simba kupindua pindua mambo na kukiuka makubaliano ya awali.
Ikumbukwe kuwa Hemed Morocco ni kocha msaidizi wa Taifa Stars na TFF tayari
walishampa ruhusa ya kwenda kufanya kazi Simba kwa barua rasmi.
Kwa mujibu wa Morocco amesema hiyo ni kazi kama
kazi nyingine tofauti na ambavyo Simba wanafikiria kwasababu yeye
atatumia muda wake na ujuzi wake kwa ajili ya kuwasaidia wao lakini
kwasababu wameshindwana, ameamua kurudi nyumbani kwake Zanzibar na hana
tena haja na kibarua hicho hata kama Simba watafikia kiwango hicho cha
mshahara alichokita mwanzo.
Post a Comment