0
 Muda mchache ujao kwenye dimba la Taifa Jijini Dar es salaam panatarajiwa kuwa na mchezo wa ligi kuu tanzania bara baina ya klabu ya Simba ya jijini humo almaarufu wekundu wa msimbazi dhidi ya maafande wa JKT RUVU waliohamisha maskani yao kutoka pale mkoani Pwani na kuyahamishia Mlalakuwa jijini Dar.

Kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuwa wa vuta nikuvute kutokana na matokeo ya timuzote mbili kwenye michezo yao iliyopita simba imemrudisha benchini mshambuliaji wake Paul Kiongera ambaye alikua jukwaani kwenye mchezo dhidi ya wakatamiwa wa Mtibwa.

Licha ya kumrejesha benchini mshambuliaji Paul Kiongera lakini kikosi cha simba kinatarajiwa kuzikosa huduma za mshambuliaji wake machamchari Ibrahim Ajibu ambaye anatajwa kuwa majeruhi mara baada ya kuchezewa rafu mbaya na kiungo mkongwe aliyewahi kukipiga kwa mafanikio makubwa kwenye klabu hiyo ya Simba Henry Joseph Shindika.

Kikosi cha simba kinachotarajiwa kuanza kwenye mchezo wa leo ni;

1. Vincent Angban
2. Hassan Isihaka
3. Juuko Murdish
4. Emery Nimubona
5. Mohammed Tshabalala
6. Justice Majabvi
7. Jonas Mkude
8. Mwinyi Kazimoto
9. Hamis Kiiza
10. Danny Lyanga
11. Peter Mwalyanzi

Kikosi cha Akiba

1. Peter Manyika
2. Hassan Kessy
3. Abdi Banda
4. Said Ndemla
5.Joseph Kimwaga
6. Raphael Kiongera
7. Mussa Mgosi

Post a Comment

 
Top