0
Wawakilishi wa mshambuliaji wa klabu ya PSG ya nchini Ufaransa Edinson Cavan wamekutana na kufanya mazungumzo na mabosi wa klabu ya Manchester United imefahamika.

Kwa mujibu wa mtandao wa ESPN, wa nchini Marekani umedai kuwa wawakilisha hao wa mshambuliaji huyo wa klabu ya Paris Saint-Germain wamekutana na mabosi wa mashetani wekundu hao kwaajili ya kuzungumzia mpango unaotajwa sasa wa klabu ya Man Utd kutaka kumsajiri mshambuliaji huyo.

United wanahusishwa na kutaka kumsajili Cavani kwa muda mrefu sasa na taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo yenye makazi yake jijini Paris ni kuwa Mruguay huyo kwa sasa anataka kuondoka kwenye viwanja vya  Parc des Princes ili ajiunge na mashetani wekundu hao waliochini ya mkufunzi Louis van Gaal.

Bosi wa klabu ya PSG Mfaransa  Lauent Blanc amauambia mtandao wa ESPN alipokua akifanya mahojiano nao kuwa Cavani amekua akichezeshwa kwenye nafasi tofauti na nafasi yake ya asili kutokana na ndani ya klabu hiyo kuwepo mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic jambo ambalo linamfanya kukosa raha ndani ya klabu hiyo.

Post a Comment

 
Top