Mshambuliaji wa klabu ya TP Mazembe Mbwana Samatta ambaye pia ni mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani yuko nchini Ufaransa kwenye mazungumzo yenye nia ya kutaka kukamilisha uhamisho wake wa kwenda kujiunga na klabu ya Olympique
Marseille.
Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania tayari yuko kwenye mji wa Marseille kwaajili ya mazungumzo ya mwishomwisho ili aweze kusajiliwa na klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya nchini Ufaransa.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari hizi ni kuwa klabu hiyo ya nchini Ufaransa inataka kuhakikisha inapambana na muda wa dirisha la usajili wa mwezi huu wa Januari kabla halijafungwa kuhakikisha kuwa wanaziba nafasi ya mshambuliaji Micky Matshuayi anayetajwa kuwaniwa na klabu ya West Ham United ya nchini Uingereza.
Klabu ya RC Genk imetajwa kuwa katika hatua nzuri ya kuhakikisha inamnasa mfungaji bora wa michuano ya vilabu bingwa barani Afrika na tayari walisha sainiana mkataba wa awali na Mbwana anayetajwa kuwa na thamani ya Euro milioni moja ambayo klabu ya Marseille inatajwa kuwa tayari kutoa kiasi hicho cha pesa.
Samatta ameisaidia klabu ya TP mazembe kutwaa ubingwa wa CAF kwa ngazi za vilabu akiwa mfungaji bora wa michuano hiyo ameichezea klabu hiyo jumla ya michezo 103 na kufunga magoli 120.
Post a Comment