0
Kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Niyonzima ameanza mazoezi na wenzake leo baada ya uongozi kukubali msamaha aliouomba mchezaji huyo wiki iliyopita.

Niyonzima amesema anajisikia furaha kumaliza matatizo yake na uongozi na sasa anarudi kuwatumikia Wanayanga ambao kwa muda mrefu walikosa mchango wake hadi timu inamaliza mechi za mzunguko wa kwanza.

“Nafurahi kurudi tena kundini kwasababu ni mengi yamesemwa lakini nafurahi kwa nafasi hii nyingine najua mchezo mashabiki walikasirika lakini naomba radhi tena na watarajie mambo mazuri kutoka kwangu sasa,”amesema Niyonzima.

Naye kocha Hans van der Pluijm amemkaribisha kundini mchezaji huyo na kumtaka kufanya kazi ya ziada ili kupigania nafasi ya kucheza kwani wachezaji waliopo wapo kwenye viwango vya juu kwasasa na haoni wa kumweka benchi.
 
“Mimi sina shida na Niyonzima, ni mchezaji wangu na alikuwa anafanya vizuri sana kwa kipindi chote alichokaa hapa klabuni nipo tayari kufanya naye kazi kama atakuwa amemalizana na uongozi masuala yake ya utovu wa nidhamu,” amesema Pluijm.

Niyonzima alisimamishwa na klabu hiyo kutokana na utovu wa nidhamu na baadaye ikatangazwa kuwa mkataba wake umevunjwa, lakini hivi karibuni aliomba msamaha na kuna taarifa kuwa ameshasamehewa na uongozi wa timu hiyo.

Post a Comment

 
Top