Baada ya taarifa kuzagaa mitandaoni kwamba Katibu Mkuu wa Yanga Dr.
Jonas Tiboroha ameachia ngazi kwenye uongozi wa klabu hiyo, yeye
amejitokeza na kupinga taarifa hiyo akiita ni uvumi na uzushi
unaosambazwa na watu ambao wanaongea vitu wasivyovijua.
Dr. Tiboroha amethibitisha kwamba yeye bado ni kiongozi halali wa
klabu ya Yanga wakati akihojiwa leo asubuhi (January 20) kwenye kipindi
cha michezo cha E-FM Radio.
“Nashangaa, hizo taarifa sijui zinatoka wapi, lakini niwahakikishieni
kwamba, ikitokea kitu kama hicho kinatokea basi mimi mwenyewe nitakuwa
mtu wa kwanza kuongea.
Kila mtu kwenye klabu anashangaa haelewi kwamba
huo uvumi umeanza namna gani lakini mimi nafikiri inaweza kuwa ni mbinu
za watu kutaka kuleta mustakabali usioleweka katika klabu yetu”, amesema
Dr. Tiboroha.
“Mimi nafanya kazi yangu kama ninavyopaswa kufanya haya mengine
yanakuja namna gani mimi sielewi, lakini binafsi nachoelewa ni kwamba
kama ni kuondolewa kuna taratibu hata viongozi wangu hawajawahi
kuniambia kitu kama hicho, hata wao wanashangaa kuona mambo kama hayo
yanatokea kwenye magazeti”.
“Sasa ninachotaka kusema ni kwamba, sijui chanzo cha hizo habari
kinatoka wapi na siwezi kujua motives ya hizo taarifa ni nini au lengo
lao wanaozisambaza hizo taarifa wanataka kufanya nini.
Kwanza niliona
kwenye mtandao nikihusishwa na mgogoro wa Niyonzima baadaye ikawa
imepotea nafikiri ni watu haohao wanaongea vitu wasivyovijua”.
Baada ya kuwepo kwa uwezekano mkubwa wa kiungo wa klabu hiyo Haruna
Niyonzima kurejeshwa kwenye kikosi cha Jangwani, kuna taarifa zimekuwa
zikizagaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba huenda Dr. Tiboroha akaamua
kutimka kwenye klabu hiyo.
Post a Comment