Klabu ya Real Madrid imemzuia mshambuliaji Cristiano Ronaldo kutembelea Morocco imethibitika.
Taarifa zinadai kuwa mshambuliaji huyo wa klabu hiyo amezuiliwa kuendelea na tabia yake ya kuuwa na safari za mara kwa mara za nchini Morocco na Rais wa klabu ya Real Madrid Florentino Perez.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii kimedai kuwa sababu kuu iliyomfanya Rais wa klabu hiyo afikie maamuzi hayo magumu ni kutokana na kuporomoka kwa kiwango cha mshambuliaji huyo kwa siku za hivi karibuni hali ambayo kwa mujibu wa Perez ndio ambayo imesababisha timu hiyo kuto kuwa na matokeo ya kueleweka kwenye michezo yake ya mashindano mbalimbali.
Ronaldo amekua akitorokea nchini Morocco mara kwa mara kwa minajili ya kwenda kumtembelea rafiki yake wa karibu Badr Hari,
akitajwa kuwa na tabia ya kuondoka kila siku baada ya kumaliza mazoezi ya asubuhi na kurejea Madrid nyakati za jioni.
Katika katazo hilo alilolifanya Perez amemthibitishia Ronaldo kuwa kutoka kwa rafiki yake mkubwa Mohamed VI ambaye ndiye mfalme wa Morocco atajulishwa kila mara ambapo Ronaldo atakua akienda Morocco na hivyo kuwa rahisi kumchukulia hatua za kinidhamu.
Post a Comment