0

Arsenal imetajwa kuwa ndio klabu inayoingiza kipato kikubwa zaidi miongoni mwa vilabu vyote barani Ulaya na Ulimwenguni kwa ujumla kwenye mapato yatokanayo na pesa za viingilio vya uwanjani kwenye viwanja vya nyumbani.

Kwa maana hiyo Arsenal imeipiku klabu ya Chelsea miongoni mwa vilabu vya jiji la London kuwa klabu inayoingiza pesa zaidi kwenye kila mchezo unaochezwa kwenye dimba lake la nyumbani.

Hii inakuja kwa mara ya kwanza kabisa katika kipindi cha miaka sita tangu klabu ya Arsenal ilipoanza kuutumia uwanja wake mpya wa Emirates mnamo mwaka 2006.

Mapato haya ya ziada yamekuja kutokana na klabu ya Arsenal kuutumia uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua takribani watu 61,000 umeifanya Arsenal kuwa ndio klabu inayoingiza pesa nyingi zaidi miongoni mwa vilabu vyote barani Ulaya na Duniani kwa ujumla.

Arsenal inaingiza wastani wa kiasi cha paundi milioni 101.84 kwa kila mchezo tofauti na klabu ya Real Madrid, inayoingiza wastani wa kiasi cha paundi milioni 100.12 katika kila mchezo inaocheza kwenye dimba la santiago Bernabeu, wakati Barcelona, yenyewe inaingiza wastani wa kiasi cha paundi milioni 90.17 kwenye kila mchezo inaoucheza kwenye dimba la Nou Camp.
Manchester United iko katika nafasi ya nne kwa wastani wa maingizo ya paundi milioni 87.96 kwenye kila mchezo unaochezwa kwenye dimba la Old Trafford wakati Chelsea iko katika nafasi ya sita na pato la wastani wa paundi za Uingereza milioni 71.84 inayozipata kila inapocheza kwenye dimba la Stamford Bridge.

Liverpool inaingiza wastani wa kiasi cha paundi milioni 57.85 na iko katika nafasi ya nane kwenye orodha hiyo, wakati  Manchester City iko katika nafasi ya tisa ikiingiza kipato cha wastani wa kiasi cha paundi milioni 43.98  na Tottenham iko katika nafasi ya kumi kwenye orodha hiyo na kipato chake cha wastani wa paundi milioni 41.83.

Post a Comment

 
Top