0

Mshambuliaji Fernando Torres usiku wa jana alitoka kwenye ushujaa mpaka mlaumiwa kwenye mchezo wa timu yake ya Atletico Madrid dhidi ya klabu ya Barcelona pale timu hiyo ilipopoteza mchezo wa awali wa robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa jumla ya magoli 2:1 ikishuhudia mshambuliaji huyo mkongwe akizawadiwa kadi nyekundu.

Fernando Torres amesema kadi hiyo nyekundu aliyoambulia mshaambuliaji huyo ambayo kwa namna moja au myingine aliighalimu timu yake ambayo mpka yeye anazawadiwa kadi hiyo ilikua inaongoza kwa jumla ya goli moja kwa bila ameizungumzia kadi hiyo na kudai kuwa ndio tukio baya kabisa alilowahi kulionja katika maisha ya mpira wa miguu.

Torres alikwenda mbali zaidi na kulilaumu shirikisho la soka barani Ulaya UEFA kwa kushindwa kuwapanga waamuzi wenye viwango vinavyoendana na ukubwa wa mechi yenyewe.

Post a Comment

 
Top