Klabu ya Majimaji ya mjini Songea leo hii itajitupa kwenye dimba lake la nyumbani la Majimaji kutupa karata yake kwa mara nyingine tena itakapokuwa inawakabili klabu ya Coastal Union kutoka jijini Tanga kwenye mwendelezo wa michezo ya ligi kuu ya Tanzania bara.
Majimaji inajitupa ugani ikwa na kumbukumbu nzuri ya matokeo waliyoyapata kwenye mchezo wao wa mwisho waliocheza kwenye dimba lao hilo la nyumbani dhidi ya klabu ya Mbeya City kutoka jijini mbeya ambapo Majimaji walipata ushindi wa jumla ya magoli 3:1.
Akizungumza na kipindi cha michezo leo kinachorushwa na 93.0 Jogoo Fm ya mjini Songea kinachorushwa mishale ya saa moja na nusu kwa saa za Afrika ya Mashariki kocha wa timu hiyo Kally Ongara amesema wao wako kamili kuhakikisha wanapata matokeo mazuri kwenye mchezo huo na matokeo mabaya waliyoyapata Coastal Union kwa kufungwa jumla ya magoli 4:1 dhidi ya klabu ya Mbeya City na yale ya wao kuwafunga Mbeya City jumla ya magoli 3:1 hayawafanyi wao kubweteka kuelekea kwenye mchezo huo.
Nae daktari wa timu ya Majimaji Shaabani Mboto amesema kuwa kikosi cha Majimaji kikokamili na mchezaji Mamir ambaye alikua anasumbuliwa na Malaria amerejea kikosini hivyo ni jukumu la mwalimu Ongara kumjumuisha kikosini mchezaji huyo kama ataona inafaa kufanya hivyo.
Klabu ya Majimaji inazihitaji sana alama tatu za mchezo wa leo ili iweze kujihakikishia kucheza ligi kuu msimu ujao haswa ikizingatiwa kuwa klabu hiyo ina ratiba ngumu sana ya michezo kwenye raundi hii ya pili kwani mpaka sasa bado haijacheza mchezo hata mmoja wa marejeano dhidi ya vigogo wa soka la Bongo Simba, Yanga na Azam.
Pos | Team | P | W | D | L | GS | GA | +/- | Pts | |
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
1 | Simba | 24 | 18 | 3 | 3 | 43 | 13 | +30 | 57 | |
2 | Young Africans | 22 | 16 | 5 | 1 | 54 | 12 | +42 | 53 | |
3 | Azam | 22 | 15 | 6 | 1 | 38 | 14 | +24 | 51 | |
4 | Mtibwa Sugar | 23 | 12 | 6 | 5 | 28 | 16 | +12 | 42 | |
5 | Tanzania Prisons | 25 | 10 | 10 | 5 | 22 | 20 | +2 | 40 | |
6 | Mwadui | 24 | 9 | 7 | 8 | 23 | 21 | +2 | 34 | |
7 | Stand United | 25 | 10 | 4 | 11 | 22 | 22 | +0 | 34 | |
8 | Mbeya City | 25 | 7 | 6 | 12 | 27 | 33 | -6 | 27 | |
9 | Toto Africans | 25 | 6 | 9 | 10 | 23 | 34 | -11 | 27 | |
10 | Maji Maji | 24 | 7 | 6 | 11 | 16 | 33 | -17 | 27 | |
11 | Ndanda | 24 | 5 | 11 | 8 | 20 | 24 | -4 | 26 | |
12 | Kagera Sugar | 25 | 6 | 7 | 12 | 19 | 28 | -9 | 25 | |
13 | Ruvu Stars | 24 | 6 | 6 | 12 | 24 | 37 | -13 | 24 | |
14 | JKT Mgambo | 25 | 5 | 8 | 12 | 20 | 31 | -11 | 23 | |
15 | African Sports | 26 | 5 | 5 | 16 | 10 | 30 | -20 | 20 | |
16 | Coastal Union | 25 | 4 | 7 | 14 | 14 | 35 | -21 | 19 |
Post a Comment