0
Mwanamasumbwi Manny Pacquiao amesema miezi 11 aliyokaa nje ya ulingo akiuguza majeraha yake mara baada ya kupoteza pambano lake dhidi ya Mmarekani Floyd Mayweather kilikua ni kipindi kigumu sana katika maisha yake ya ubondia kulikoni atakapokua anatangaza kustaafu siku atakapomaliza pambano lake la mwisho dhidi ya Tim Bradley siku ya jumaapili.

Manny mwenye umri wa miaka 37 amesisitiza kuwa mara baada ya pambano hilo atasaafu mchezao huo wa masumbwi mara baada ya pambano bila ya kujali matokeo yatakayojitokeza kwenye pambano hilo dhidi ya  Bradley, na kudai kuwa mawazo yake na maisha yake sasa anayahamishia kwenye masuala ya kisiasa nchini kwao ambako anataka kugombea nafasi ya kuwa Seneta.


Post a Comment

 
Top