Mashabiki wa mpira wa miguu duniani wametoa heshima zao za mwisho kwa aliyekua mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa Italy na klabu ya AC Milan Cesare
Maldini, wakiongozwa na wachezaji wazamani wa vilabu mbali mbali vya nchini Italy kwenye mazishi ya ligendari huyo.
|
Ligendari wa timu ya taifa ya Italy na AC Milan, Paolo Maldini akisindikizwa na mke wake Adriana Fossa kwenye mazishi ya baba yake. |
Mtoto wa ligendari huyu Paolo, aliongoza mamia ya waombolezaji waliojumuika kutoa heshima zao za mwisho pamoja na mama yake mzazi Marisa kwenye viwanja vya mtakatifu Ambrose jana asubuhi.
|
Maldini (kulia) akitoka uwanjani na mwanawe Paolo baada ya timu ya taifa ya Italy kupoteza mchezo na kutolewa kwenyehatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la Duniaya mwaka 1998 nchini Ufaransa. |
Maldini,
ambaye ameshinda mataji manne ya Serie A na moja kombe la European Cup akiwa na wana Rossoneri
(AC Milan) kati ya mwaka 1954 na 1963, amefariki akiwa na umri wa miaka 84 siku ya jumaamosi.
|
Mlinzi na nahodha wa zamani wa klabu ya Inter Milan Javier Zanetti nae alikuwepo kwenye zoezi la kutoa heshima za mwisho. |
|
Clarence Seedorf kocha na mchezaji wa zamani wa klabu ya AC Milan akiwasili eneo la tukio. |
Post a Comment