Wachezaji wa Simba Hamisi Kiiza na Juuko Murshid, wote raia wa Uganda
huenda wakasimamishwa na kukatwa mshahara na uongozi wa timu hiyo baada
ya wachezaji hao kuchelewa kurudi nchini kujiunga na wenzao baada ya
pambano la kufuzu fainali za mataifa ya Afrika dhidi ya Burkina Faso.
Msemaji wa Simba Hajji Manara ameiambia Goal,
wachezaji hao walipewa ruhusa ya siku tano iliyokuwa ikiisha Jumamosi
lakini hadi sasa hawajarudi nchini na wanajiandaa kuwashitaki TFF, na
kuwachukulia hatua za kinidhamu pindi watakapo rudi.
“Tunachojua walishamaliza majukumu ya timu ya taifa na hatuna taarifa
yoyote kuhusu kuchelewa kwao kwani hata kocha wetu Jackson Mayanja
amewasiliana na kocha mkuu wa timu ya taifa Uganda Cranes’ ameshangwaza
na taarifa hizo za kutorejea kwa wachezaji hao,”amesema Manara.
Manara kushindwa kurejea kwa wakati huo ni utovu wa nidhamu na
watahakikisha wanalichukulia hatua swala hilo ili liwefundishwa kwa
wengine wenye matarajio ya kufanya hivyo.
Tayari kocha Mayanja, amewaondoa wachezaji hao kwenye programu yake
kwa ajili ya kuwakabili Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa robo
fainali ya Kombe la Shirikisho utakaofanyika Aprili 11 Uwanja wa Taifa
Dar es Salaam.
Chanzo: Goal.com




Post a Comment