0
Klabu ya Azam Fc inatarajia kumkosa beki wake wa pembeni mwenye uwezo wa kucheza kama kiungo mkabaji Shomary Kapombe kwenye michezo yote miwili ya  Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) dhidi ya Esperance ya Tunisia.

Tayari Kapombe amekosa mechi mbili mfululizo za Ligi Kuu timu hiyo ikitoa sare zote, 1-1 dhidi ya Toto Africans ya jijini Mwanza Jumapili na jana imetoa sare ya jumla ya magoli 2-2 dhidi ya Ndanda hapo jana kwenye dimba la Chamazi9, Na beki huyo wa zamani wa klabu za Simba na AC Cannes ya nchini Ufaransa 
anatarajiwa kusafirishwa leo kwenda Afrika Kusini kwa matibabu.

Daktari wa Azam FC, Juma Kwimbe amethibitisha kwamba Kapombe hatacheza mechi zote dhidi ya Esperance Jumapili jijini Dar es Salaam na wiki mbili zijazo Tunis kwa sababu ni mgonjwa.

“Amekuwa akilalamika kuumwa mbavu kiasi cha kulia wakati mwingine, jana ikabidi afanyiwe vipimo na imegundulika anasumbuliwa na Nimonia, hivyo leo anakwenda Afrika Kusini kwa matibabu,”amesema. 

Kukosekana kwa Kapombe katika kikosi cha Azam FC wakati huu ambao timu ipo kwenye vita ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho ni pigo.

Mbali na kuwa mhimili imara wa safu ya ulinzi, Kapombe pia amekuwa mpishi na mfungaji mzuri wa mabao ya timu msimu huu, hadi sasa akiwa amefunga mabao saba kwenye Ligi Kuu pekee.

Post a Comment

 
Top