Kenya imeshuka hatua 12 kwenye msimamo wa viwango vya FIFA vilivyotolewa mwezi huu huku Tanzania ikishuka kwa hatua 5 kwenye orodha ya viwango vya ubora wa soka ya Fifa iliyotolewa leo.
Kenya kwa sasa imeporomoka mpaka namba 115 huku Tanzania ikishuka mpaka namba 130.
Harambee Stars wameshuka baada ya kushindwa mechi mbili za kufuzu kwa Kombe la Mataifa Bingwa Afrika na Guinea Bissau.
Taifa hilo la Afrika Magharibi limepanda hatua 45 hadi nambari 102. Guinea
Bissau waliichapa Kenya 1-0 mechi ya kwanza tarehe 23 Machi na kwenye
mechi ya marudiano wakashinda tena 1-0 jijini Nairobi.
Tanzania haijahesabiwa mechi yoyote ya karibuni. Walishinda 1-0 dhidi
ya Chad mechi ya kwanza ugenini lakini Chad wakajiondoa na
hawakushiriki mechi ya marudiano jijini Dar es Salaam.
CAF ilifuta
matokeo hayo dhidi ya Chad katika kundi G.
Miongoni mwa
mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Uganda inaongoza ikiwa nambari
72, Rwanda inafuata nambari 87, Kenya nambari 115, Burundi nambari 122,
Tanzania nambari 130 na Sudan Kusini nambari 155.
Orodha ya mataifa kumi bora Afrika ni kama ifuatavyo:
- Algeria
- Ivory Coast
- Ghana
- Senegal
- Misri
- Cape Verde
- Tunisia
- Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
- Guinea
- Congo
Duniani, orodha ya kumi bora ni kama ifuatavyo:
- Argentina
- Ubelgiji
- Chile
- Colombia
- Ujerumani
- Uhispania
- Brazil
- Ureno
- Uruguay
- England
Post a Comment