Mfanyabiashara maarufu wa kiarabu Dk Sulaiman Al-Fahim
ametangazwa kuwa mwenyekiti mtendaji wa klabu ya African Lyon ambayo
itashiriki ligi kuu ya Tanzania Bara msimu ujao.
Mmiliki wa klabu ya African Lyon, Rahim Kangezi amethibitish
kuwa wamemuomba Al Fahim kushika nafasi hiyo kutokana na uzoefu wake
katika michezo hasa mpira wa miguu mbali ya kuwa mfanyabiashara bilionea
katika nchi za Uarabuni na duniani kwa ujumla.
Kangezi amesema Al Fahim ni Rais wa kampuni ya Arab
Union for Real Estate Development ya Dubai na miaka ya nyuma alikuwa
msemaji wa kampuni inayomiliki klabu tajiri duniani, Manchester City,
Abu Dhabi United Group (ADUG). ADUG iliinunua Manchester City Septemba,
2008.
Pia Al Fahim alitaka kununua klabu ya Portsmouth
ambayo ilikuwa inashiriki ligi kuu ya Uingereza, lakini mpango huo
haukuweza kukamilika.
Kangezi
amesema kuwa Al Fahim ataanza kazi rasmi Aprili 16 ambapo atatangaza
timu yake ambayo atafanya nayo kazi katika kuibadili klabu hiyo na kuwa
klabu bora Tanzania na bara la Afrika.
Post a Comment