Nahodha wa Yanga Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amesema yupo fiti
kukabiliana na straika hatari wa wapinzani wao hao, Mgabon, Malick
Evouna, ambaye ndiye mchezaji hatari kwa upande wa timu ya Al Ahly.
Cannavaro amesema yupo fiti kwa asilimia
kubwa baada ya kushiriki mazoezi kikamilifu ya timu hiyo kwenye kambi ya
Pemba na anataka kuanza ili kuonyesha uwezo wake kwa kuwafunga Ahly
kama alivyofanya mwaka 2014, walipofanya hivyo walipokutana nayo uwanja
wa taifa na kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
“Ni mchezo mkubwa na mgumu lakini ukweli sina hofu hata kidogo
kwasababu mazoezi niliyofanya yamenipa uhakika kamba naweza kuwamudu Al
Ahly, na kuonyesha uwezo mkubwa kama inavyo fahamika,”amesema Cannavaro.
Kocha Hans van der Pluijm wa Yanga huenda akamuanzisha Cannavaro
kwenye pambano hilo la michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika lililopangwa
kupigwa Jumamosi Aprili 9 uwanja wa taifa Dar es Salaam.
Post a Comment