0



Neymar hatacheza tena katika michuano ya Copa America msimu huu akiwa na Brazil.

Hiyo inatokana na mchezaji huyo kufungiwa mechi nne kutokana na kitendo chake cha kumpiga beki wa Clombia na mpira tena kwa makudusi baada ya mwamuzi kupuliza kipenga cha mwisho.

Pia ilielezwa kwamba Neymar alimsemea maneno machafu mwamuzi Enrique Osses wakati wakiingia vyumbani.

Hali hiyo ilisababisha Neymar alambwe kadi nyekundu, lakini adhabu hiyo, imeongeza machungu zaidi kwake.

Pamoja na mechi hizo nne, Neymar kapigwa faini ya dola 10,000.

Post a Comment

 
Top