KIPA Ivo Mapunda amekubali kuongeza mkataba wa mwaka mmoja kuichezea
klabu ya Simba msimu ujao baada ya uongozi wa timu hiyo kuridhishwa na
kiwango chake msimu huu uliomalizika.
Mapunda ameuambia mtandao huu amefuraishwa na uongozi wa
timu yake kuwa na imani naye na kumuongeza mkataba mpya na atahakikisha
anaweka historia kubwa kwenye timu hiyo pindi aatakapo maliza kipindi
chake cha kuichezea Simba.
“Nifurai kuona bado uongozi na benchi la ufundi wameendelea kuniamini
na mimi nitahakikisha najiandaa ili kuipa ubingwa wa ligi ya Vodacom
msimu ujao timu yangu ili iwe shukrani kwa mashabiki wote wa
Simba,”amesema Mapunda.
wala hana papara ya usajili katika klabu yake ya Simba kwani mabosi
wake wamemuahidi kumuongezea mkataba ambao mwenyewe anataka uwe wa miezi
18 tu.
Ivo Mapunda alitua Simba msimu wa 2013/14 akitokea Gor Mahia ya Kenya
na kuwa chaguo la kwanza kwa makocha wote walioifundisha timu hiyo
akiwemo Zdravko Logarusic,Patrick Phiri na Goran Kopunovi
Post a Comment