Kamati ya
utendaji ya Shirikishi la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Katika kikao chake cha
leo pamoja na mambo mengine ilipitia mwenendo wa Timu ya Taifa (Taifa Stars)
ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mchezo kati ya Tanzania na Uganda, kama sehemu ya
tathmin ya mwenendo wa timu mchezo ambao umekemilika kwa stars kufungwa jumla ya magoli 3:0.
Kamati ya
utendaji kwa kauli moja imeamua yafuatayo:
1.Ajira ya
Kocha Mkuu Maart Nooij inasitishwa mara moja kuanzia tarehe 21/June/2015.
2.Benchi
lote la ufundi la Taifa stars limevunjwa kuanzia tarehe 21/06/2015.
3.Uongozi
wa TFF utatangaza punde benchi jipya la ufundi la timu ya Taifa.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Post a Comment