Dennis Bergkamp alisajiliwa na Meneja wa wakati huo wa Arsenal Bruce Rioch kwa ada ya paundi milioni 7.5mnamo mwezi June 1995.
Alikuwemo kwenye kikosi cha Arsenal cha msimu wa 1997-1998 kilichoshinda Premiership kama kombe hilo lilivyokua likijulikana kwa wakati huo.
Alifunga goli ambalo linakumbukwa sana na mashabiki wengi wa soka ulimwenguni kwenye mchezo amba Arsenal ililazimisha sare ya jumla ya magoli 3-3
dhidi ya Leicester mnamo mwaka 1997, kinachokumbukwa zaidi ni ufundi aliouonesha Bergkamp kabla ya kumfunga mlinda mlango Kasey Keller.
Mshambuliaji huyu wa zamaniwa Arsenal alikua msingi imara kwa timu hiyo pale alipoiongoza timu hiyo kuivurumisha klabu ya Everton jumla ya magoli 4-0 na kutangwazwa rasmi kuwa mabingwa wa ligi mnamo May 1998.
Katika kipingi cha muongo mmoja (miaka 10) aliyokaa na klabu ya Arsenal, Bergkamp amefuga jumla ya magoli 120 katika michezo 423 aliyoshiriki katika mshindano mbalimbali akiwa na klabu ya Arsenal.
Mshambuliaji huyu alipewa jina la utani la 'Non-Flying Dutchman' yaani Mdachi asiyeruka kutokana na uwoga wake wa kupanda Ndege.
Aliingia kwenye orodha ya wachezaji wa Arsena waliofunga magoli 100 mnamo mwezi January 2003 pale alipofunga kwenye mchezo dhidi ya klabu ya Oxford United kwenye dimba la Highbury.
Mnamo mwaka 1998 Bergkamp alitajwa kuwa mchezaji bora wa mwaka.
Amewahi kutajwa kuwa mchezaji bora wa mwezi kwa vipindi vinne tofauti katika miaka tofauti lakini mara ya kwanza kabisa ilikua mnamo mwezi August 1997, September 1997, March 2002 na February 2004.
Mara mbili amewahi kuwa miongoni mwa wachezaji watatu bora wa FIFA wa dunia akimaliza katika nafasi ya tatu ya mchezaji bora wa mwaka wa FIFA na alijumuishwa kwenye orodha ndefu ya wachezaji 125 bora ambao wako hai mpaka sasa akitajwa katika nafasi ya 100 katika orodha hiyo.
Bergkamp anashikilia nafasi ya 11 katika orodha ya wafungaji wa magoli mengi wa klabu ya Arsenal akiwa ameifumgia timu hiyo jumla ya madoli 120 katika kipindi chote alichokua na klabu hiyo.
Alishinda kombe la FA mnamo mwaka 2005 baada ya Arsenal kuwafunga Manchester United
magoli 5-4 kwa penati mara baada ya kutoka sare ya 0-0katika muda wa kawaida na wanyongeza.
Post a Comment