Wenyeji Chile waliweka kando sakata ya ajali ya gari ya nyota wao
Arturo Vidal akiwa amelewa na kupambana kuhakikisha kuwa wanaingia robo fainali ya ya michuano ya Copa Amerika
kwa kuwararua Bolivia jumla ya magoli 5-0 usiku wa jana.
Charles Aranguiz alifunga magoli mawili huku nyota Alexis Sanchez,
Gary Medel na goli la kujifunga mwenyewe kutoka kwa Ronald Raldes
wakikamilisha sherehe hiyo.
Vidal alikamatwa na kushtakiwa kwa kuangusha gari lake la kifahari
aina ya Ferrali akiwa katika mwendo kasi baada ya kushiriki vileo katikatukio linalotajwa kutishia nafasi ya wenyejihao kufuzu kwaajili ya hatua inayofuata ya michuano hiyo.
Ushindi huo ulisaidia Chile kumaliza juu katika Kundi A na kupata nafasi ya kufuzu kwaajili ya hatua ya robo fainali Jumatano ijayo dhidi ya timu ya tatu bora zaidi katika
makundi yote ambayo kwa sasa inaonekana kuwa mabingwa Uruguay au
Paraguay.
Post a Comment