0
Lundo la majeruhi lialoikabili klabu ya Arsenal hasa sehemu ya kiungo limeifanya klabu hiyo kumfikiria kiungo wa klabu ya Bayer Leverkusen, Lars Bender ambaye kwa taarifa kutoka ndani ya klabu yake nae pia ni majeruhi.


Arsenal inamfikiria Bender kufuatia kuumia kwa kiongo Francis Coquelin, Lakini hata hivyo kiungo huyo raia wa Ujerumani anatajwa kuwa anasumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu.



Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo  zimethibitisha kuwa tayari Bender amekwisha fanyiwa upasuaji uliokwenda salama ili kulitatua tatizo hilo linalomkabili na sasa anatarajiwa kuwa nje ya uwanja mpaka mwishoni mwa mwezi huu wa desemba.

Taarifa iliyotolewa kwenye mtandao wa klabu ya Leverkusen imesema "Lars Bender amefanyiwa upasuaji wa kifundo chake cha mguu wa kulia kwenye mji wa Basel hapo jana na anatarajiwa kubakia nchini Switzerland kwa wiki moja zaidi na baada ya hapo ndio atarejea mjini Leverkusen kwaajili ya kuendelea kuuguza jeraha lake.

Post a Comment

 
Top