0

Kocha wa Simba, Mwingereza Dylan Kerr amesema anatakakuona ushindani wa namba katika kila idara ndani ya kikosi chake kuanzia kwenye mazoezi hadi mechi za Ligi ya Vodacom zinazotarajia kuanza tarehe 12 ya mwezi huu.

Kerr raia wa Uingereza ameiambia Goal, ushindani itakuwa ndiyo njia pekee itakayosaidia kuwapa matokeo mazuri nakupigania ubingwa wa Tanzania bara msimu huu.

“Timu yoyote bora lazima iwe na ushindani kuanzia mazoezini hadi kwenye mechi hapo ndipo kunakopatikana mafanikio ya mchezaji na timu kwa ujumla ndiyo maana nataka kuona ushindani huo ukihamia Simba,” amesema Kerr.

Kama ukiwa na watu wanaoshindana kwa ajili ya maendeleo, basi lazima maendeleo yatapatikana ndani ya kikosi,” alisema.

Simba chini ya Kerr, inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi ya Vodacom ikiwa na pointi 21 katika mechi tisa walizocheza na imeweza kupoteza mechi mbili tu jambo ambalo kocha huyo anaamini wanaweza kufanikiwa kupata mafanikio.

Post a Comment

 
Top