KLABU ya soka ya Chelsea imewasilisha
maombi ya mpango wa kuupanua Uwanja wa Stamford Bridge ili kuweza
kuingiza Mashabiki 60,000.
Iwapo kutapitishwa ujenzi huo majengo yaliyo jirani na uwanja huo yatalazimika kuvunjwa ili kupisha ukarabati huo.
Chelsea, walianza kutumia uwanja wa Stamford Bridge tangu 1905 ambapo mara ya mwisho kukarabatiwa na kupanuliwa ilikua ni katika Miaka ya 1990 na kuufanya uwe na uwezo wa kuchukua watazamaji 42,000.
Post a Comment