KLABU ya Yanga imetamba kushinda mechi zake zote tatu kabla
haijakwenda Tunisia kurudiana na Etoile du Sahel katika michuano ya
Kombe la Shirikisho Afrika CAF.
Msemaji wa Yanga Jerry Muro ameiambia mtandao huu wanataka
kwenda Tunisia wakiwa tayari wamesha tangazwa mabingwa wa Ligi ya
Vodacom Tanzania bara hivyo ili kutimiza lengo hilo wanalazimika
kushinda mechi hizo tatu.
“Tunajua ugumu uliopo katika mechi hizo lakini hakuna
kinachoshindikana tuna kikosi imara ambacho naamini kitapambana na
kupata pointi hizo 9 ambazo zinatufanya twende Sousse Tunisia tayari
tukiwa mabingwa wapya uzuri na mechi hizo tunazitumia kama mazoezi
kujiandaa na mchezo dhidi ya Etoile du Sahel,”amesema Muro.
Timu ambazo zitakutana na Yanga ni Stand United iliyocheza nayo leo
kwenye dimba la taifa Dar es Salaam kisha itacheza na Ruvu Shooting na
na mechi ya tatu itapambana na Azam FC, kabla ya kuanza safari ya
kurudiana na Etoile pambano ambalo litapigwa Mei 1 huko Tunisia.
Post a Comment