Kamati ya Rufaa ya Shirikisho la soka Tanzania TFF iliyokutana Aprili
19, 2015 imepanga kusikilizwa kwa rufaa ya Damas Ndumbaro Mei 10 mwaka
huu, makubaliano ambayo yalifikiwa na pande zote mbili kwa pamoja.
Kikao hicho kilipitisha taratibu za kisheria ambazo zitatumika kuamua
kesi hiyo, ambazo ni taratibu kama zinazotumika mahakamani ikiwemo
kuwasilisha hoja kwa mdomo na si maandishi, kitendo ambacho kimekubaliwa
na pande zote mbili.
Utaratibu huu umekua ukitumika katika mahakama za kawaida kuepusha manung’uniko kwa upande mmoja kulalamika umeonewa.
TFF ilimsimamisha Ndumbaro kwa kipindi cha miaka saba kutojihusisha
na soka kutokana na kitendo chake cha kukiuka maadali ya Shirikisho hilo
kwa kuvipa ushirikiano vilabu kutokana na makato ya asilimia tano ya
fedha za udhamini.
Post a Comment