KOCHA Goran Kopunovic wa Simba amesema kukosekana kwa mshambuliaji wa
Kiganda kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City ndiko kuliko sababisha
wakapoteza mechi hiyo iliyokuwa muhimu kwao.
Kopunovic ameiambia mtandao huu kuwa pamoja na kufanya
vizuri kwa washambuliaji Ramadhan Singano na Ibrahim Ajib lakini
wapinzani wao walikosa mtu wa kumuhofia na kuamua kufanya mashambulizi
mengi kwenye lango lao na kufanikiwa kupata ushindi huo.
“Kumkosa Okwi ili kuwa moja ya sababu iliyotugarimu na kutufanya
kupoteza mchezo wa Mbeya City kwa mabao 2-0 kwa sababu wapinzani
walicheza bila uwoga na kwa sababu hatukuwa na mtu
wanayemuhofia,”amesema Kopunovic.
Kocha huyo amesema kesho wanacheza na Mgambo anaamini watalipa kisasi kwa kuwa Okwi atakuwepo pamoja na beki Hassan Kessy.
Post a Comment