Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” inayodhaminiwa na
bia ya Kilimanjaro Premium Lager kimekamilika baada ya kundi la pili
lenye wachezaji nane kuwasili jana mchana nchini Chad tayari kwa mchezo
wa kesho dhidi ya wenyeji kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika
(AFCON) mwaka 2017.
Kundi hilo la pili limewasili majira ya saa sita mchana (saa za Chad)
likiongozwa na mkuu wa msafara ambaye pia ni Rais za ZFA, Ravia Idarus
na kupokelewa na viongozi waliopo jijini N’Djamena.
Mara baada ya kuwasili D’jamena wachezaji walipata nafasi ya
kupumzika hotelini kabla ya kuelekea mazoezini kufanya mazoezi ya pamoja
kwa wachezaji wote, yakiwa ni mazoezi ya mwisho kabla ya mchezo wa leo.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars Charles Mkwasa amekiongoza kikosi chake
chenye jumla ya wachezaji 20 kufanya mazoezi mepesi saa 9 mchana katika
uwanja wa Idriss Mahamat Ouya uliopo jijini N’Djamena.
Katika mazoezi ya jana wachezaji wa Taifa Stars walionekana kuwa na
umakini mkubwa katika kusikiliza maelekezo ya kocha Mkwasa, huku morali
ya wachezaji ikiwa juu kuelekea kusaka pointi 3 muhimu katika mchezo
huo.
Wachezaji waliopo Chad ni magolikipa Aishi Manula na Ally Mustafa,
walinzi Shomari Kapombe, Juma Abdul, Haji Mwinyi, Mohamed Hussein, David
Mwantika, Erasto Nyoni na Kelvin Yondani.
Viungo ni Himid Mao, Jonas Mkude, Mwinyi Kazmito, Mohamed Ibrahim,
Farid Musa, Deus Kaseke na Shiza Kichuya, huku washambuliaji wakiwa ni
John Bocco, Ibrahim Ajibu, Thomas Ulimwengu na nahodha Mbwana Samatta.
Mechi kati ya Chad dhidi ya Tanzania inachezwa leo saa 9:30 (saa 11:30 kwa saa za Tanzania) katika uwanja wa
Idriss Mahamat Ouya jijini N’Djamena, na utarushwa moja moja na kituo
cha luninga cha Taifa cha Chad (Tele Chad).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment