Bosi wa klabu ya Machester United Louis van Gaal amepanga kuwatema wachezaji kadhaa waliomo kwenye kikosi cha timu yake kabla ya dirisha la usajili kufungwa kutokana na sababu mbalimbali.

Taarifa zinasema kuwa Nani, Javier Hernandez na Shinji Kagawa inaonekana kama ni miongoni mwa wachezaji ambao nafasi zao ndani ya klabu ziko mashakani katika kikosi hicho.Wengine ni Marouane Fellaini na Anderson ambao nao pia huenda wakatolewa kafara.
ikumbukwe kuwa tayari takriban wachezaji sita wa timu hii wamekwisha ondoka klabuni hapo kutokana na sababu mbali mbali.
Rio Ferdinand, Nemanja Vidic, Patrice Evra, Alex Buttner, Federico Macheda na Bebe wameondoka kutokana na sababu mbali mbali zikiwemo umri na kutafuta nafasi za kudumu mahala pengine,wakati Ryan Giggs amestaafu na kuwa msaidizi wa Van Gaal.

Van Gaal akimuangalia msaidizi wake Albert Stuivenberg akitoa maelekezo. Asubuhi ya leo Van Gaal amesema: "nimewaacha wachezaji wote wa kikosi hiki wacheze ili nipate kuwajua vyema kwani kabla ya ziara hii ni wachache sana ambao nilikua nawafahamu kinagaubaga.

Javier Hernandez (Chicharito) ni mmoja kati ya waliokalia kuti kavu
"Ili uwe na kikosi bora unahitaji kufanya mabadiriko ambayo wakati mwingine huwa yanaambatana na machungu kwa pande zote zinazohusika na timu aliongeza Van Gaal."
Post a Comment