0
Big decision to make: Arsene Wenger is looking at candidates to replace Thomas Vermaelen as club captain

Arsenal imekubali kumuuza Thomas Vermaelen kujiunga na Barcelona kwa ada ya paundi milioni 15 mara baada ya klabu ya Manchester United kukataa kumtoa Chris Smalling kama sehemu ya dili hilo.

Arsenal wanataka kumuuza Vermaelen nje ya Uingereza isipokuwa tu kama United itakua tayali kumjumuisha  Smalling kwenye dili hilo mchezaji ambaye Arsene Wenger mwanzoni alijaribu kumsajili alipokua akiitumikia klabu ya Fulham mnamo mwaka 2010.

 as_vermaelen

Mkurugenzi wa Barcelona Raul Sanllehi amesafiri kwenda jijini London kwaajili ya mazungumzo na amerejea akiwa na matumaini makubwa kwamba Arsenal na Vermaelen wataikubali ofa ya klabu ya Barcelona ya mkataba wa miaka minne na mshahara wa paundi elfu 80,000 kwa wiki.

Mbeligiji huyo anatarajiwa kufanya mazungumzo na Barcelona kwaajili ya kujadili mambo mbalimbali yahusuyo mkataba wake na Wakatalunya hao.

Vermaelen alijiunga na Arsenal mnamo mwezi June 2009 na ameitumikia klabu hiyo jumla ya michezo 150 tangu ajiunge na klabu hiyo ya kusini mwa jiji la London.

Post a Comment

 
Top