0
Feeling the heat: Brendan Rodgers takes a break as his Liverpool side prepare to face their rivals

Brendan Rodgers akiwaangalia vijana wake mazoezini.


Sahau kuhusu mchezo wa ngao ya jamii kwenye uwanja wa Wembley siku ya jumaamosi, Nchini marekani kutakua na shughuli nzito ya kudhihilisha ubora wa vikosi baina ya Manchester United na Livepool.

Mafahari hawa wawili wanapokutana kitu pekee kinachotokea ni kila mmoja kutaka kumdhihilishia mwenzake ni jinsi gani anatarajia kufanya au anafanya kwenye ligi na michuano mbalimbali.

Kiungo wa Manchester United Darren Fletcher amesema “ Ni mchezo kati ya Man Uited na Livepool. Nafahamu kuwa nimchezo wa kujiandaa na msimuna ni mashindano ya kabla ya msimu lakini Manchester United inapokutana na Liverpool siku zote huwa linakua jambo kubwa.”

 “Tunataka kushinda mchezo huu kwakua tunatambua kuwa kushinda kila mchezo kunarejesha na kuongeza ari ya timu na mashabiki”

United wana kumbukumbu mbaya ya msimu uliokwisha kwani kwenye mchezo wao wa nyumbani dhidi ya Vijogoo vya Anfield walipoteza mchezo kwa kukubali kichapo cha jumla ya goli 3:0.

Manchester imemwajiri miongoni mwa makocha bora wa kiwango cha Dunia LvG na kwenye michezo yake ya mwanzoni mwa msimu wamefanikiwa  kuzifunga klabu za LA Galaxy, AS Roma, Inter Milan na kuivurumisha Real Madrid jumla ya goli 3:1 kwenye uwanja wa Michigan ikishuhudiwa Young akifunga magoli mawili na lile moja likiwekwa kimiani na Javier Hernandez (Chicharito).


Relaxed: Van Gaal has made a real impression since joining Manchester United after the World Cup
Liverpool ilijihakikishia kucheza fainali baada ya kupata ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya AC Milan katika dimba la Charlotte shukrani kwa magoli kotoka kwa Joe Allen naSuso,Ikishuhudiwa Rickie  Lambert akikosa mkwaju wa penati kwenye mchezo huo.

Ukiachilia mbali upinzani mkubwa na wakihistori wa vilabu hivi lakini kuna kitu cha kukumbukwa kuelekea mchezo huo kuhusiana na mameneja wa timu zote mbili ambapo meneja wa klabu ya Livepool Brendan Rodgers atakutana uso kwa uso na bosi mpya wa klabu ya Manchester Louis van Gaal mtu ambaye alimkataa kuwa mkurugenzi wa ufundi wa klabu ya livepool miaka miwili iliyopita.


Louis van Gaal alifanya mazungumzo na kukubaliana na Liverpool juu ya nafasi hiyo jambo ambalo Rodges alilikataa kwa kusema ni bora afanye kazi na kundi la watu kulikoni kufanya kazi na mkurugenzi wa ufundi.

“Ni jambo ambalo lilikuwepo hapo awali kabla mimi sijaja hapa lakini mimi nahitaji kufanya kazi na kundi la watu kuliko mkurugenzi wa ufundi.”

Post a Comment

 
Top