
Katika taarifa yake kwa waandishi wa habari Lampard alisema: "Nimechukua maamuzi ya kustaafu soka la kimataifa. Ni maamuzi magumu sana kwangu mimi lakini nimekua mtu wa kutafakari sana tangu nilipotoka kwenye fainali za kombe la Dunia."
"Nimekua nikikubalika sana na kuheshimika sana mbele ya mashabiki na waalimu waliokua wakinichagua kuitumikia timu yangu mara kadhaa na kila nikitazama nyuma najaribu kujenga taswira ya furaha niliyokua nikiipata kila nilipokua nivaa jezi ya timu yangu ya taifa."
Post a Comment