
Klabu ya AC Milan inamtazama mshambuliaji Javier Hernandez (Chicharito) kama ndio mrithi sahihi wa mshambuliaji Mario Balotelli anayetimukia Anfield.
Taarifa kutoka nchini Italy zinasema kwamba Hernandez kwa sasa ndio anaongoza katika orodha ya wachezaji wanaotakiwa na klabu hiyo na meneja Louis van Gaal anaonekana kuwa radhi kutaka kumuuza mchezaji huyo Raia wa Mexico.
Hernandez, alipata nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha LVG siku ya Jumapili kwenye dimba la Old Traford mchezo ambao ilishuhudiwa United ikoambulia kichapo cha jumla ya magoli 2-1 mbele ya Swansea, lakini nafasi yake ilichukuliwa wakati wa mapumziko ma Luis Nani aliyetimukia kwa mkopo kwenye klabu ya Sporting Lisbon.
Vilabu vya Juve na Inter Milan vya huko nchini Italy vyote vimeonesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji huyo aliyeshauriwa kuachana na mashetani wekundu hao na kocha wake wa timu ya Taifa ili kuilinda nafasi yake kwenye timu hiyo.
Post a Comment