
Mikel Arteta anatarajiwa kutajwa kama nahodha mpya wa klabu ya Arsenal.Taarifa zinasema kwamba Mfaransa Arsene Wenger anajiandaa kumkabidhi unahodha Arteta kwenye klabu ya Arsenal kufuatia maamuzi ya kumuuza nahodha wake wa sasa Thomas Vermaelen.

Bosi wa The Gunners ambaye timu yake iko kwenye maandalizi makali wa mtoano wa kuwania nafasi ya kuingia kwenye makundi ya Champions League dhidi ya Besiktas ambyo mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Demba Ba ndio anakipiga kwa sasa anahitaji nahodha mpya mara baada ya Vermaelen kuwa njiani kujiunga na kati ya vilabu vya Manchester United au Barcelona.
Arteta kwa sasa ndiye nahodha msaidizi kwa sasa anapigiwa upatu sana na wadadisi wa masuala ya kisoka akifuatiwa na Mjerumani Per Mertesacker.Lakini taarifa zinasema kwamba endapo Arteta atakua nahodha basi Mertesacker ndiye atakayekuwa nahodha wako.
Post a Comment