Mshambuliaji wa timu ya taifa ya
ujerumani, Miroslav Klose, ambaye aliweka rekodi ya kihistoria kwa kuwa
mfungaji bora katika michuano ya kombe la duni mwaka 2014, baada ya
kufunga mabao 6 peke yake, ametangaza kuustaafu
Mchezaji huyo wa klabu ya Lazio ya huko nchini Italy, mwenye umri wa miaka 36,
ameeleza kwamba anastaafu baada ya ndoto yake ya utotoni kukamilika,
ikiwa ni pamoja na ushindi wa timu ya taifa ya ujerumani nchini Brazil,
ambayo ilitwaa kombe la dunia. Klose amesema michuano hiyo ya kombe la
dunia iliyompa sifa hatoisahau maishani mwake.

Klose ni mchezaji wa pili wa Ujerumani kutangaza kustaafu katika
ngazi ya kimataifa baada ya ushindi wa timu ya taifa ya Ujerumani nchini
Brazil. Nahodha wa timu ya taifa ya Ujerumani, Philipp Lahm, mwenye
umri wa miaka 30 alitangaza kustaafu siku 5 baada ya fainali kati ya
Ujerumani na Argentina, jambo ambalo liliwaacha watu wengi vinywa wazi.
Klose ameweka rekodi ya kuwa mfungaji bora katika michuano ya kombe
la dunia (mabao 16), ambayo ilikua inashikiliwa na Christian Ronaldo wa
Brazil, ambaye alifunga mabao 15 kwenye guu lake katika michuano kama
hiyo.
“Kwa kweli Miro, alionesha ujuzi wake na alitoa mchango mkubwa kwa timu ya taifa ya Ujerumani”,
amesema Meneja wa timu ya taifa ya ujerumani Joachim Löw, akibaini
kwamba anaheshimu uamzi wa Miroslav na mchango aliotoa kwa timu ya
taifa.

"Katika masuala ya soka na utu, tutamkumbuka Miroslov”, amemalizia Löw, akinukuliwa kwenye mtandao wa shirikisho la soka la Ujerumani (DFB).
Rais wa shirikisho la soka nchini Ujerumani, Wolfgang Niersbach,
amebaini kwamba Klose hakua tu mchezaji tofauti na wengine, alikua pia
mtu wa kuigwa.
“Kufuatia mabao 71 aliyofunga akiichezea timu ya taifa ya
ujerumani na mabao 16 aliyofunga katika michuano ya kombe la dunia,
ameweka rekodi mbili muhimu ambayo itampelekea kupata na fasi ya heshima
katika kitabu cha kihistoria", amesema Niersbach.

Ifuatayo ni orodha ya mabao yote 16 ya mshambuliaji huyo kwenye michuano mbalimbali ya Dunia.
1, 2, 3: Germany 8-0 Saudi Arabia, hatua ya makundi kombe la Dunia-2002
4: Germany 1-1 Republic of Ireland, hatua ya makundi kombe la Dunia-2002
5: Cameroon 0-2 Germany, hatua ya makundi kombe la Dunia-2002
6, 7: Germany 4-2 Costa Rica, hatua ya makundi kombe la Dunia-2006
8, 9: Ecuador 0-3 Germany, hatua ya makundi kombe la Dunia-2006
10: Germany 1-1 Argentina nusu fainali kombe la Dunia-2002
11: Germany 4-0 Australia, hatua ya makundi kombe la dunia-2010
12: Germany 4-1 England, hatua ya 16 bora kombe la dunia-2010
13, 14: Argentina 0-4 Germany, nusu fainali kombe la Dunia-2010
15: Germany 2-2 Ghana, hatua ya makundi kombe la Dunia-2014
16: Brazil 1-7 Germany, nusu fainalikombe la dunia-2014
Post a Comment