0
Wanted man: Arsenal defender Thomas Vermaelen could join rivals Manchester United this summer
  • Thomas Vermaelen huenda akawa mchezaji wa saba kutoka klabu ya Arsenal kutua ndani ya jiji la Manchester. Taarifa rasmi ambayo ntandao huu imezinasa zinasema Arsene Wenger amemruhusu mchezaji huyo kujiunga na mashetani wekundu wa  Manchester.

    Mlinzi huyo anatarajia kuwa mchezaji wa sita kutua jijini Manchester kama masuala yake ya uhamisho yatakwenda sawasawa kutokana na ukweli kwamba anawindwa kwa udi na uvumba na Meneja mpya wa klabu ya Mancester United mholanzi Louis van Gaal.

    Arsene Wenger amekusanya kiasi cha paundi milioni 96 kwa kuwauza nyota kadhaa wa Arsenal kwenda kwa vilabu hivi viwili vikubwa kutoka jijini Manchester japo swali la msingi linalosalia vichwani mwa wadadisi wengi wa masuala ya soka ni je Mfaransa huyo alikua sahihi kufanya mauzo ya baadhi ya wachezaji wenye vipaji vikubwa kama wao?

    Still smiling? Arsene Wenger has sold a number of players to United and Manchester City in recent seasons, but was he right to do so?
    Thomas Vermaelen huenda akawa mchezaji wa saba kutoka klabu ya Arsenal kutua ndani ya jiji la Manchester. Taarifa rasmi ambayo ntandao huu imezinasa zinasema Arsene Wenger amemruhusu mchezaji huyo kujiunga na mashetani wekundu wa  Manchester.


    1.EMMANUEL ADEBAYOR

    Alinunuliwa kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 7 kutoka AS Monaco mnamo mwaka 2006 na kuuzwa kwa kitita cha paundi milioni 25 mwaka 2009 kwa klabu ya Manchester City.

    Alipotua Arsenal alipachikwa jina la "Babby kanu" akifananishwa na kiungo Mnigeria aliyewahi kuitumikia klabu hiyo Nwanko Kanu. 

    Lakini alishindwa kabisa kuisaidia timu yake kushinda kikombe chochote ndani ya misimu mitatu aliyokua na Arsenal na kumbukumbu pekee kubwa atakayosalia nayo ni kufungiwa michezo minne kwenye msimu wa ligi wa mwaka 2006-2007 baada ya kukwaruzana na kiungo wa klabu ya Chelsea Frank Lampard kwenye mchezo wa fainali ya kombe la ligi.

    Alisaini mkataba wa miaka mitano na City amabapo ni miaka mitatu tu akiitumikia klabu hiyo na kipindi kilichosalia akikitumia kwa mkopo kwenye vilabu mbali mbali barani Ulaya.

    Hapo pia hakufanikiwa kushinda kikombe chochote pale na kitu pekee anachobakia kama kumbukumbu nacho ni kushangilia kwa kuuzunguka uwanja mzima mbele ya mashabiki wa klabu yake ya zamani ya arsenal na pia kufungiwa michezo mitatu kwa kitendo chake cha kumpiga teke la makusudi usoni mshambuliaji wa wakati huo wa Arsenal Robin van Persie.
     
    2. GAEL CLICHY'
     
    Alinunuliwa kutoka klabu ya AS Cannes ya huko nchini Ufaransa kwa ada ya paundi 250,000 mnamo mwaka 2003 ambapo Mzee Wenger alijibebesha jukumu la kwenda nyumbani kwake mjini  Tournefeuille nchini Ufaransa na kumsahwishi ajiunge na klabu hiyo akimuandaa kuwa mrithi wa Ashely  Cole. Aliuzwa mwaka 2007 kwa ada inayokaliliwa kuwa paundi milioni 7 ambapo mara baada ya kuondoka alisema maneno mabaya sana dhidi ya Arsenal kama ilivyokua kwa Nasri.

    3. ROBIN VAN PERSIE
     
    Alinunuliwa kwa kitita cha paundi milioni 2.75 kutoka klabu ya Feyenoord ya huko nchini Uholanzi. Misimu yake minane aliyokuwa ndani ya Arsenal ilikua na safari ndefu yenye milima na mabonde kwani katika karia yake alikua akisumbuliwa na maumivu ya mara kwa mara licha ya kuwa ni mmoja kati ya washambuliaji hodari ulimwengumi. 

    akiwa Arsenal alifanikiwa kutwaa taji la FA mwaka 2005 na Ngao ya jamii mwaka 2004 na pia alikua mfungaji bora wa klabu kwa takribani misimu minne kati ya nane aliyo kuwepo Arsena.Katika msimu wake wa mwisho akiwa na Arsenal alikua mfungaji bora kabla ya kuushangaza ulimwengu na kuamua kutimkia United. Aliuzwanamo mwaka 2012 kwa ada ya paundi milioni 24.

    Akiwa United aliendeleza makali yake kwani msimu wa mwanzo tu kutua klabuni hapo aliifungia timu hiyo magoli 26 yaliyoisaidia kutwaa taji la ligi kuu nchini Uingereza na Ngao ya jamii.

    4.BACARY SAGNA
     
     Alinunuliwa kwa kitita cha paundi milion 6 kutoka Auxerre ya Ufaransa mnamo mwaka 2007 na kutumia takribani miaka 7 akiwa na Arsenal. Alikua sehemu ya kikosi cha Arsenal kilichotwaa kombe la FA msimu uliopita. Ameondoka bure ndani ya kikosi hicho mara baada ya kumaliza kandarasi yake.

    Amesaini mkataba wa miaka mitatu na Man City kandarasi inayokwenda kumpa mshahara wa paundi 150,000 kwa wiki ikiwa ni mara dufu zaidi ya paundi milioni 60,000 alizokua akilipwa na klabu ya Arsenal.

    "Nataka niweke wazi baadhi ya mambo hapa. tayari nilishakua nimefungasha kila kitu tayari kwa safari maana siku zote nilikua nafikiri kuhusu umri wangu, Mshahara wangu lakini sijakaa misimu yote ndani ya klabu ya Arsenal nikipata mshahara unao fanana. Sio tu kwaajili ya pesa hapana pia nilikua na kila sababu ya kuyabadili mazingira yangu."

    5. SAMIR NASRI

     Alinunuliwa kwa kitita kinachokadiliwa kuwa paundi milioni 15 kutoka kalabu ya Marseille ya huko nchini Ufaransa mnamo mwaka 2008. Hapa pia Mzee Wenger akiutumia vyema Ufaransa wake kumshawishi kijana kujiunga na Arsenal kijana ambaye Wafaransa walikua wakimuona kama Zidane wao mpya.
     
    Alilazimika kuuzwa kwa klabu ya Manchester City manamo mwaka 2011 kwa ada ya paundi milioni 11 mara baada ya kugoma kusaini mkataba mpya na washika bunduki hao.

    Ndani ya hajapata nafasi ya kucheza kama vile ilivyokua ndani ya klabu  ya Arsenallacha ya kuwa mmoja kati ya wachezaji ambao wameisaidia timu hiyo kushinda vikombe na kufanya mapinduzi mbali mbali katika tasnia ya mpira wa miguu.

    5.KOLO TOURE

    Alinunuliwa kwa kitita cha paundi 150,000 mnamo mwaka 2002 kutoka klabu ya ASEC Abidjan. Alinunuliwa kwa minajilia ya kutumika kama kiungo mkabaji na mlinzi wa pembeni lakini mzee Wenger aliamua kumtumia kama mlinzi wa kati nafasi amabayo anaonekana kuitendea haki haswa msimu wa 2003-2004 ambapo ushirikiano wake na Soul Campbell uliifanya Arsenal imalize msimu ikiwa haijafungwa mchezo hata mmoja.

    Aliuzwa mwaka 2009 kwa klabu ya Manchester City kwa ada ya paundi milioni 16 na akiwa na City ameiwezesha kutwaa ubingwa wa ligi kuu, FA na Ngao ya jamii. Lakini anasalia na kumbukumbu mbaya kichwani mwake ya kufungiwa kucheza soka kwa miezi sita mnamo mwaka 2011 mara baada ya kugundulika kuwa alikua akitumia madawa yaliyopigwa marufuku michezoni
     


Post a Comment

 
Top