
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina alisajiliwa na klabu ya Manchester United siku 12 zilizopita na United ilimtambulisha rasmi siku ya Ijumaa mbele ya waandishi wa habari.
Lakini mpaka sasa mchezaji huyo aliyenunuliwa kutoka klabu ya Sporting Lisbon kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 16 hajaitumikia klabu yake hiyo mpya.

Ziko taarifa zinazodai kuwa Rojo ameingia
kwenye matatizo sawa na yaliyokua yanawakabili Waajentina wenziwe
Carlos Tevez na Javier Marschelano ya kumilikiwa na mtu wa tatu ambaye ni
wakala wake, Umiliki ambao alianza kumilikiwa akiwa anacheza nchini
Ureno. Lakini pia ziko taarifa zinazodai kuwa mchezaji huyo hajalitumikia taifa lake michezo ya kutosha yenye
kumuwezesha kupata kibali cha kufanya kazi mara moja.
Lakini imethibitika kuwa
jambo halisi linalo chelewesha kupatikana kwa kibali cha Rojo ni
kuendelea kusubiri kutoka kwa maofisa wa ubalozi wa nchini Uhispania
Visa itakayomwezesha Rojo kuishi na kufanya kazi nchini Uingereza.

Taarifa zinadai kuwa maofisa hao wanajaribu kupitia kwa kina mafaili ya mchezaji huyo yaliyoko nchini kwao Ajentina kutokana na kuwepo kwa nyaraka ndani ya mafaili hayo zinao onesha kutokea kwa mzozo baina ya Rojo na majirai zake wa huko nchini Argentina mnamo mwaka 2010.
Rojo hajawahi kusimamishwa mahakamani lakini kesi hiyo bado iko kwenye uchunguzi baada ya kesi kufunguliwa upya mwezi wa tano mwaka huu.
Rojo
hana rekodi za uharifu lakini maofisa wa ubalozi wanajaribu kuzipitia takwimu kwa undani kabla ya kuamua kumpa kibali mchezaji huyo.

Rojo alikua na mahojiano na maafisa wa ubalozi na bado yuko nchini Uhispania na anasubiria majibu ya masaili yake hayo.
Mabosi wa klabu ya Manchester United wanaonekana kuweka moyo ndani ya jokofu wakati wakisubirisha majibu ya kutoka kwa maofisa ubalozi hao na rasmi wameandika kwenye mtandao wa klabu hiyo kuwa: "Marcos ameondoka kuelekea nchini Uhispania ili kufanyiwa mahojiano na maafisa ubalozi na hatimaye kupatiwa visa ambayo ndiyo atakayoitumia kuingilia nchini Uingereza ili apate kibali cha kufanya kazi nchini humu hii ni kawaida."
Post a Comment