0
Patient: Samuel Eto'o has turned down the chance to sign for Ajax as he awaits other offersLiverpool imetangaza rasmi kuwa iko kwenye hatua za mwisho za kufanya mazungumzo yenye nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Samuel Eto'o.

Liverpool ambayo iko katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa mshambuliaji mtukutu wa Kiitaliano anayekipiga ndani ya klabu ya AC Milan, Mario Balotelli katika kile kinachoonekana kama uimarishaji wa kikosi cha meneja Brendan Rodgers.

Eto'o ambaye yuko huru kwa sasa mara baada ya mkataba wake wa awali kumalizika akiwa na matajiri wa jiji la London Chelsea kwenye majira haya ya joto ameonekana kuvivutia vilabu kadhaa vya barani Ulaya, Marekani na Mashariki ya kati.

Liverpool offer Eto'o one-year deal

Taarifa zinasema kuwa binafsi Mkamerooni Samwel Eto'o anapendelea kubakia Uingereza ili aendelee kukipiga kwenye Premier League.

Ajax na Everton zote kwa pamoja zimeonesha nia ya kutaka kumsajili Eto'o, lakini Liverpool inaonekana ikiwa katika nafasi mzuri ya kuinasa saini ya mshambuliaji huyo aliyewahi kukipiga kwenye vilabu kadhaa vyenye sifa Duniani vikiwemo Barcelona, Inter Milan, Real Malloca na Real Madrid.

Liverpool imempa Samwel Eto'o ofa ya mkataba  wa mwaka mmoja utakao mpatia kiasi cha paundi 93,000 kwa wiki mkataba ambao utahusisha na bonasi kutokana na uwezo atakao uonesha uwanjani lakini pia kuongezewa mkataba kwa mwaka mmoja zaidi iwapo tu ataonesha uwezo wa hali ya juu ambao utawavutia mabosi wa ndani ya Anfield.

Endapo Eto'o na Balotelli wataungana tena ndani ya Liverpool itakua ni mara ya pili kwa wawili hao ufanya kazi pamoja kwani tayari wawili hawa wameshawahi kufanya kazi kwa pamoja misimu kadhaa iliyopita wakiwa kwenye klabu ya Inter Milan ya hoko nchini Italy.

Post a Comment

 
Top