0


 Done: Eliaquim Mangala has signed for Manchester City from Porto in £32million dealManchester City hatimaye wamekamilisha uhamisho wa mlinzi wa timu ya taifa ya Ufaransa anayekipiga kwenye klabu ya Fc Porto Eliaquim Mangala, kwa dau la paundi milioni 32.
 
Mchezaji huyo ameondoka leo hii kwenye uwanja wa ndege wa  Le Bourget  nchini Ureno kuelekea jijini Manchester kwaajili ya kufanyiwa vipimo vya afya ili aweze kujiunga rasmi na matajiri hao wa jiji la Manchester.
Mangara anatarajiwa kujiunga na walinzi wengine Muargentina Martin Demichelis na nahodha wa timu hiyo Mbeligiji Vicent Kompany kwaajili ya kuimarisha sehemu ya ulinzi ya vijana wa Manuel Pellegrin.

Landed his man: Manuel Pellegrini identified the centre of defence as a problem area for the champions 

Dili hili limecheleweshwa kwa takribani mwezi mmoja sasa limefikiwa muafaka rasmi leo hii na Mangara sasa anakwenda kuungana mchezaji mwenzake aliyetoka kwenye klabu ya Porto Fernando ndani ya kikosi cha Manchester City kukamilisha idadi ya mchezaji wa sita kusajiliwa na City kwenye majira haya ya kiangazi.

"Nina mipango ndio maana niko hapa, Nina furaha kubwa kuja nchini Uingereza kwakuwa kwangu mimi EPL ndio ligi bora Duniani kwakuwa ina ushindani mkubwa na kadri siku zinavyokwenda inakua na mapinduzi makubwa.

"Lakini Fernando naye amenishawishi sana kuja hapa kwani muda mfupi aliokaa hapa amekua akiniambia mengi mazuri yaliyopo ndani na nje ya klabu kitu ambacho kwa namna nyingine kimenishawishi mimi kuja hapa."

 "Lakini pia uwepo wa watu ambao nina wafahamu ndani ya timu hii imekua ni chachu nyingine kwangu mimi kuja hapa kuitumikia timu hii, wako watu kama  [Bacary] Sagna, [Gael] Clichy and [Samir] Nasri."

Post a Comment

 
Top