0

Mlinzi wa kushoto wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Spoting Lisbon ya huko Ureno Marcos Rojo ameiandikia klabu yake kuilazimisha imuuze kwenda klabu ya Manchester United.

Klabu ya Southampton ni moja kati ya vilabu vya Premier League ambavyo vilikua vikimuwania mchezaji huyo kabla ya klabu ya United kutuma ofa kwenye klabu ya Sporting Lisbon. 

Bosi wa southampton Ronald Koeman amesema "Tulikua tukimuhitaji Rojo lakini masuala ya uhamisho ni kazi ya Mwenyekiti Les Reed ambaye ndiye mtendaji mkuu wa klabu yetu" 

Pia Rafael Benitez meneja wa klabu ya Napoli naye amamuwania  Rojo aende akacheze kwenye Serie A lakini bosi wa Manchester United Louis van Gaal anatarajia kuwazidi kete ili kuongeza ushindani upande wa kushoto wa timu ya Manchester ambako Luke Shaw anatarajia kutawala. 

Rojo hajafanya mazoezi na  Sporting hii leo ambapo Manchester United wanajiandaa kuweka ofa ya paundi milion 16 ili kumnasa kinda huyo wa Kiargentina.

Post a Comment

 
Top