Kiungo wa Azam FC, Brian Majwega ameliomba Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF), kumpa ruhusa ya kuitumikia klabu ya Simba ili
kulinda kipaji chake.
Kiungo huyo raia wa Uganda alipeleka barua TFF akiilalamikia Azam kwa
kushindwa kumlipa mshahara kwa miezi sita lakini anashangaa sasa
inamwekea kauzibe ili asijiunge na Simba.
Mchezaji huyo mwenye uwezo wa juu wa kupiga mipira iliyokufa amekuwa
akifanya mazoezi na Simba kwa siku kadhaa hali iliyozua mtafaruku mkubwa
kati ya Simba na Azam.
Majwega ambaye anadaiwa kusajiliwa na Simba kwa dau la Sh milioni 40,
lakini bado kuna figisufigisu kwani Azam ambayo ilimpeleka kwa mkopo
KCCA ya Uganda kudai bado ni mchezaji wake.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii kimesema kuwa Majwega alisema kuwa ni
vyema, TFF ikaliwekea uzito suala lake hilo kwa kulisikiliza kwa haraka
kabla ya dirisha la usajili kufungwa ili kuondokana na tatizo alilonalo.
“Lengo langu ni kucheza soka na nimejipanga kuhakikisha nakuwa
mchezaji mzuri na kuleta ushindani katika timu yangu na hata katika timu
tutakazokutana nazo.
“Nawaomba TFF kuhakikisha wanalisikiliza suala langu kwa haraka zaidi
ili niweze kuwa huru na kujiunga na timu nyingine,” alisema Majwega."
Aidha, kwa upande wa Katibu Mkuu wa Azam, Idrissa Nassoro,
alipoulizwa juu ya mchezaji huyo, alisema Majwega bado ni mchezaji wao
kwa kuwa aliondoka huku akiwa bado na mkataba.
Kiungo huyo alisaini mkataba wa miaka miwili na Azam na unatarajiwa kumalizika mwakani.
Kiungo huyo alisaini mkataba wa miaka miwili na Azam na unatarajiwa kumalizika mwakani.
Post a Comment