MSHAMBULIAJI wa Stand United Elias Maguri amesema
anaweza kujiunga na timu yoyote, lakini siyo Simba ambayo ilimdhalilisha
kwa kusema hana kiwango cha kuichezea timu hiyo.
Maguri amesema hataki kurejea Simba na zaidi anafikiria
kwenda kucheza soka nje ya Tanzania endapo atashindwa kusajiliwa na timu
nyingine za ndani.
“Ukweli siwezi tena kurudi Simba kutokana na tulivyoachana nipo
tayari kuchezea timu nyingine yoyote laki siyo wao na kwa sasa nina mtu
ambaye ananisimamia, huyo ndiye anazungumzia mambo yangu,”amesema.
Maguri ndiye anaongoza kwa mabao katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara hivi akiwa amefunga mabao tisa katika mechi 10 alizocheza Stand
United ikiwa ni muda mfupi tangu alipoachwa na Simba.
Post a Comment